Wasanii wa Twanga Pepeta muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Leaders. |
Shughuli jukwaani. |
Wanenguaji wa kike wake wakiwasili kwa mbwembwe. |
Safu ya wanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta wakiongozwa na Kiongozi wao, Luiza Mbutu, Hamis Kayumbu 'Amigolaus' na Dogo Rama. |
BENDI ya muziki wa dansi ya The African Stars Twanga Pepeta juzi uziku ilifanya uzinduzi wake wa albamu ya 11 uliofana ambapo ulifanyika katiwa viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo ambapo wasanii wakadhaa walinogesha ulipendeza na kuwa wa aina yake.Uzinduzi huo ambao uliambatana na michuano ya soka ambayo ilifahamika kama ‘Twanga Festival’ timu ya Daladala Camp ndiyo walioibuka vinara na kujipatia zawadi ya sh. 100,000.
Aidha uzinduzi huo pia ulipambwa na wasanii mbalimbali wanaotamba hivi sasa katika tasnia ya muziki na wenye majina hapa nchini kama Barnaba, Amini, Mataluma, Isha Masauzi na kundi la Mashauzi Classic.

Pia bendi ya Schengen Academy ainayoongozwa na mwanamuziki Liver Hassan na Prince Dully Skes walikuwepo kutia nakshi uzunduzi huo.
Albamu hiyo ambayo inakwenda kwa jina la ‘Dunia Daraja’ ina nyimbo sita ambazo ni majina na watunzi wake kwenye mabano ni ‘Dunia Daraja’ iliyotungwa na Charlz Baba, ‘Penzi la Shemeji’ umetungwa na Prince Muumini Mwinjuma .
‘Mtoto wa Mwisho’ umetungwa na Dogo Rama naye Kiongozi wa bendi Luza Mbutu ametunga wimbo unaokwenda kwa jina la ‘Umenivika Umasikini’ huku Kiongozi Msaidizi Saleh Kupaza ametunga wimbo wa ‘Kiapo cha Mapenzi’ na wimbo ‘Kauli’ uliotungwa na muimbaji mahiri Rogart Hegga kabla hajaihama bendi hiyo.
Majina ya albamu zingine ni ‘Kisa cha Mpemba’ (1999), ‘Jirani’( 2000), ‘Fainali Uzeeni’ (2001), ‘Chuki Binafsi’ (2002), ‘Ukubwa Jiwe’ (2003), ‘Mtu Pesa’ (2004), Safari 2005 (2005), ‘Password’ (2006), ‘Mtaa wa Kwanza’ (2007) na ‘Mwana Dar es Salaam’ (2009).
No comments:
Post a Comment