Tangazo

December 20, 2011

Kiongozi Korea Kaskazini afariki dunia

Kim-Jong il aliyefariki dunia (kushoto), na mwanae anayemrithi Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-il amefariki dunia kwa mshtuko wa moyo katika umri wa miaka 69, vyombo vya habari vya serikali vimetangaza.

Mamilioni ya raia wa Korea Kaskazini ‘wamegubikwa na huzuni isiyoelezeka’, Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema. Watu wameonekana wakilia katika mji mkuu Pyongyang.

Mwanae Kim Jong-un ameelezewa na KCNA kama "mrithi mkuu " ambaye wakorea kaskazini hawana budi kumuunga mkono na kuwa nyuma yake.

Jirani wa Pyongyang wako katika hali ya tahadhari. Taarifa ambazo hazijathibitshwa kutoka Korea Kusini zinasema Korea Kaskazini imefanya majaribio ya nyuklia Jumatatu.

Shirika la habari la Yonhap mjini Seoul lillisema kombora la nyuklia la masafa mafupi lilitupwa pwani ya mashariki ya nchi hiyo maskini iliyojitenga na yenye kumiliki nyuklia Jumatatu lakini haikujulikana haraka iwapo jaribio hilo linahusiana na tangazo la kifo cha Kim Jong-il.

    "Huu unaweza kuwa mwanzo wa mabadiliko kwa Korea Kaskazini"

William Hague, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza

Korea Kusini imeweka silaha zake kwa tahadhari baada ya tangazo hilo, ikisema nchi hiyo ilikuwa kwenye mgogoro unaofukuta. Serikali ya Japan imefanya mkutano wa dharura.

Uhusiano wa China na Korea Kaskazini na ubia katika biashara wameonyesha kushtushwa na habari za kifo hicho na kuahidi kuendeleza na kuimarisha "mchango wake was amani na utulivu katika rasi ya ukanda huu ."

Masoko ya hisa ya Asia yalishuka baada ya habari hizo kutangazwa.
 
Kilio cha sauti

Tangazo la kifo cha Kim Jong-il lilitolewa kwa kusomwa taarifa yenye hisia kupitia televisheni ya Taifa.

Mtangazaji, akiwa na mavazi meusi, alijitahidi kuzuia machozi wakati akisema alikufa kutokana na kufanya kazi za nguvu na kiakili kupita kiasi.

Baadaye shirika la habari la KCNA likaripoti kuwa alikufa kutokana na "maumivu makali ya kifua yaliyoambatana na mshtuko wa moyo (myocardial infarction)" saa mbili na nusu muda wa huko siku ya Jumamosi (23:30 GMT Ijumaa).

Wakati huo alikuwa kwenye treni katika moja ya ‘safari zake elekezi vijijini’, KCNA lilisema.

Shirika hilo la habari la serikali limesema mazishi yatafanyika Pyongyang tarehe 28 Disemba na Kim Jong-un ataongoza kamati ya mazishi. Muda wa maombolezo kitaifa umetangazwa kuanzia tarehe 17 to 29 Disemba.

Picha kutoka ndani ya taifa hilo lenye tahadhari kubwa zilionyesha watu mitaani Pyongyang wakilia baada ya taarifa za kifo hicho.

Wanachama wa chama tawala katika moja ya kijiji cha Korea Kaskazini walionyeshwa na televisheni ya Taifa wakipiga mesa na kulia kwa sauti, Shirika la habari la AFP limeripoti.

"Siwezi kuamini. Ataondokaje namna hii? Tunafanyeje sasa?" mmoja wa wanachama anayeitwa Kang Tae-Ho alinukuliwa akisema.

Mwingine, Hong Sun-Ok, alisema:"alijaribu kufanya kazi kwa bidii kufanya maisha yetu kuwa bora na ametuacha hivi tu."

KCNA linasema watu "walikuwa wakitetemeka kwa uchungu na kukata tamaa," kwa kuondokewa namna hii, lakini wataungana nyuma ya mrithi wake Kim Jong-un.

No comments: