Tangazo

December 22, 2011

MKATABA WA UJENZI WA MABASI YAENDAYO KWA HARAKA DAR (DARTS) WASAINIWA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS )Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto)  pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya  Mkandarasi M/S STRABAG INTERNATIONAL GmbH ya Ujerumani, Heribert Schippers (kulia) wakitiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Usafiri Haraka wa Mabasi jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza, Kandarasi wa Kwanza (Barabara) katika makao Makuu ya Wizara ya Ujenzi Nov.22.2011. Mradi huo wa  Ujenzi  unafadhiliwa  kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambapo mradi mzima wa kazi utagaharimu shilingi 240.9 Bilioni. Ujenzi wa awamu ya kwanza  unahusisha ujenzi wa barabara unaofikia kilometa20.9 katika barabara ya Morogoro(kutoka Kimara hadi Kivukoni (Feri), barabara ya Kawawa (kutoka) Magomeni hadi Morocco ) na barabara ya Msimbazi (kutoka Fire hadi makutano ya Nyerere -KAMATA).  Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli , Viongozi wa TAMISEMI, Wizara ya Fedha na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli akionyesha baadhi ya  ramani yenye michoro ya barabara za juu (Flying- Over) zitakazojengwa jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS )Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto)  pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya  Mkandarasi M/S STRABAG INTERNATIONAL GmbH ya Ujerumani Heribert Schippers (kulia) wakibadilishana hati za  mkataba baada ya kusaini.

No comments: