Wanamuziki wa bendi ya Twanga Pepeta, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Ubalozi na wenyeji wao kabla ya kuanza kwa shoo hiyo. |
Mwimbaji wa bendi hiyo, Amigo Las, akishambulia jukwaa na Mnenguaji wake, Shalla Pova. |
Mashabiki wakijimwaga ukumbini humo, wakati wa shoo hiyo. |
Shalla Pova, akishambulia jukwaa. |
Mkaanga Chips wa bendi hiyo, Martine Kibosho, wakiwakilisha kwa kuzicharaza drums vilivyo. |
Na Freddy Macha
BENDI ya African Stars “Twanga Pepeta” walikuwa kivutio cha sherehe za miaka 50 ya Uhuru London juzi Jumamosi baada ya kushambulia jukwaa kwa shoo yao ua nguvu na kuwapagawisha mashabiki lukuki waliojitokeza kushuhudia shoo hiyo.
Bendi hiyo iliwasili nchini Uingereza kwa mwaliko maalum wa Urban Pulse kwa kushirikiana na Jestina George pamoja na Ubalozi wa Tanzania Jijini London.
Watanzania wa kila rika, nasaba na taaluma walifurika toka miji ya Leeds, Bristol, Birmingham, Northampton, Milton Keynes na vitongoji mbalimbali kufurahia vigongo vya bendi hili lenye makao makuu Mango Garden Kinondoni Dar es Salaam.
Ukumbi wa Club 2000 Banqueting Suite ulioko nyuma ya uwanja maarufu wa Wembley ulishuhudia tafrija hiyo wakati viongozi rasmi wa serikali walipofungua tafrija wakicheza nyimbo maarufu za Kitanzania kama ule wa mwanamuziki Salum Abdallah (“Wanawake wa Tanzania” na “Tujenge Nchi Yetu”) marehemu alizoimba mara baada ya Uhuru mwaka 1961.
Viongozi waliojumuika walikuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, Balozi wetu Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, naibu wake Mheshimiwa Chabaka Kilumanga na Ofisa Habari ndani ya ubalozi,Mheshimiwa Amos Msanjila aliyehamasisha wageni kwa kunyofoa kinywaji cha “champagne” mahsusi kuzindua maadhimisho.
Akiwakaribisha wote Balozi Kallaghe alisema sherehe za miaka 50 ni idhinisho kuwa Tanzania ni nchi ya amani inayostahili kuwa fahari yetu sote.
“Waangalie Waingereza wanavyoorodhesha tarehe na mida ya majengo yao muhimu, Kutambua na kusherehekea muda kamili wa matukio ya jamii ni jambo muhimu na la kawaida,” alikumbusha kiongozi huyo na kupigiwa makofi.

No comments:
Post a Comment