Tangazo

December 1, 2011

VODACOM YAZINDUA HUDUMA YA UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA MAHUSIANO KUPITIA SIMU ZA MKONONI


Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom Tanzania, imezindua huduma ya 'Young Africa Live' itakayowawezesha wateja wake kupata taarifa sahihi za afya, mahusiano na Mapenzi kuanzia leo Desemba Mosi mwaka huu.

Kupitia huduma hiyo ya kwanza nchini wateja wa Vodacom watapata fursa ya kuunganishwa moja kwa moja na wadau wa masuala ya afya na mahusiano ya jinsia ikiwa ni pamoja na kujibiwa maswali watakayokuwa wakiuliza kupitia simu zao mkononi.

'Young Africa Live' ni huduma inayowaunganisha wanajamii kihabari kupitia simu za mkononi na kutoa burudani na fursa ya mazungumzo na kubadilishana taarifa  na uzoefu katika mada za mapenzi, ngono, mahusiano, jinsia na afya ya uzazi.

“Tunaimani kwamba huduma hii itasaidia jamii hususan vijana ambapo kupitia taarifa za kiafya wataweza kuwa na mahusiano yenye tija na kujikinga na maambuzkizi ya virusi vya Ukimwi na Ukimwi”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza.

“Kila juhudi ni muhimu katika vita ya kupunguza athari za virusi vya Ukimwi na Ukimwi, matatizo ya afya ya uzazi katika jamii ikiwemo vifo. Taarifa sahihi ni nyenzo muhimu katika mapambano haya, hivyo huduma hii ni wazi itapunguza pengo la ukosaji wa habari muhimu za afya kwa wanajamii.”Ameongeza Rene.

Ili mteja wa Vodacom aweze kunufaika na huduma hii ya kwanza nchini kutoka Vodacom anapaswa kuwa na huduma ya Intaneti kwenye simu yake na kupitia Portal ya  Young Africa Live ataunganishwa na wanajamii wengine na wadau wa afya kwa urahisi.

Gharama ndogo itatozwa kwa wateja wa Vodacom wa malipo ya kabla.

“Tunategemea vijana wengi kutumia fursa hii kujifunza, kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya masuala ya afya na mahusiano na hatimae kuwa chachu ya mabadiliko ya tabia.”Alisema Rene

Huduma ya 'Young Africa Live' imefanya vizuri katika nchi ya Afrika Kusini na kuwa tegemeo la chanzo cha habari kwa vijana ambao kupitia mazungumzo ya pamoja yameweza kuwasaidia kubadili mitazamo yao katika mapenzi, 'Ngono' na masuala ya afya ya uzazi.
        

No comments: