BAADHI YA WASHIRIKI WA MISS UTALII VYUO VIKUU 2011 KANDA YA KATI WAKIWA MAZOEZINI. |
HAWA (KULIA) NA VIOLETH WAKIWA MAZOEZINI. |
MSHIRIKI ALFONSIA NA IRINE WAKIWA MAZOEZINI. |
WASHIRIKI LILY NA LOVENESS WAKIWA MAZOEZINI. |
Kambi ya washiriki wa shindano la Miss Utalii Vyuo Vikuu 2011/12 –Kanda ya kati, imechukua sura mpya baada ya washiriki karibu wote kutambiana kutwaa taji hilo, siku ya tarehe 30-12-2011,ambayo shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa kisasa wa Club La Azziz Dodoma.
Ushindani miongoni mwa washiriki hao, ambao wanawakilisha vyuo vikuu vilivyopo mikoa ya kanda ya kati , umekuwa ni mkubwa kutokana na kila mmoja kujenga hofu dhidi ya wenzie,kutikana na ukweli kwamba karibu washiriki wote wanasifa na ubora unaokaribiana wa kutwaa taji hilo la kanda, ambapo washindi watano bora watawakilisha Vyuo Vikuu vya kanda ya kati katika fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania, zitakazo fanyika Mwezi Machi 2012.
Ari ya kila mashiriki ya kuhakikisha ushindi unakwenda katika chuo anacho kiwakilisha ni kubwa, hali inayo ashiria kuwa sasa ushindani sio baina ya washiriki tu, bali imekuwa pia baina ya vyuo vyenye wawakilishi katika shindano hilo. Ambapo lila mshiriki amekamia kukipa heshima chuo chake kwa kutwaa taji hilo la Miss Utalii Vyuo Vikuu kanda ya kati mwaka huu.
Wakizungumza na mwandishi wetu katika kambi yao ya mazoezi iliyopo katika hoteli ya NAM Dodoma,Alfonsia Victor,Loveness Shore na Getruda Meshiri na Violeth Ndawi washiriki kutoka chuo cha Mipango, walisema kuwa wamejiandaa kuhakikisha kuwa Taji linakwenda chuo cha Mipango, ili kuudhihirishia umma wa watanzania na mkoa wa Dodoma kuwa “chuo cha mipango kipo juu kielimu,michezo na hata katika kutangaza utalii wa Tanzania”.
Warembo wengine Ester Mganza, Hawa Nyange na Pendo Saimon, Lilian Maleo Lily Charles,Rebeka Nathan na Mariam Hassan toka chuo Kikuu cha Dodoma, walitamba kuwa wanauhakika taji hilo litakwenda chuo kikuu cha Dodoma, kwani ndo chuo kikubwa zaidi nchini na Afrika Mashariki na Kati, hivyo hawaoni kizuizi wala kipingamizi kwa wao kutwaa taji hilo, wamewataka wanachuo wenzao kukaa mkao wa kupokea taji hilo hivyo kuthibitisha ubora na ukubwa wa chuo chao.
Irine Richard, Martha Malakhi, Justina Kiwia,Evamery Mosha na Happynes Zawadi toka chuo cha Biashara Dodoma, wametamba kuwa taji haliwezi kwenda kwingine kokote zaidi ya CBE, kwani wao wanatoka katika chuo kikongwe na ndo chuo mama Dodoma ambacho kiko katika kitovu cha mji wa Dodoma,hivyo hawatishwi na washiriki kutoka vyuo vingine na kwamba washiriki toka CBE lazima wataibuka na Ushindi bila ya mashaka, “tunaomba wanachuo wenzetu waje kushudia tukiwachakaza washiriki toka vyuo vingine bila ya huruma.
Washiriki toka chuo kikuu cha ST John’s Dodoma Frorida Lusida ,Athunta Mathias, Miriam Zakaria na Veronika Dismas wamejigamba kuwa wao maneno ni machache wao ni vitendo tu, siku ya Ijumaa tarehe 30-12-2011 ndo itakuwa mwisho wa majigambo na tambo za washiriki kutoka vyuo vya CBE,UDOM, Uhaziri ,Uhasibu na Mipango.Mikoa ambayo vyuo vyake vinashiriki fainali hizo za kanda ni Tabora, Singida na Dodoma.
Wakati huohuo, Emmanuel Msangi ambaye ni Mratibu na Katibu Mtendaji wa Miss Utalii Tanzania Kanda ya Kati, ametaja zawadi kwa washindi kuwa ni pamoja na; Mshindi wa kwanza zawadi yenye thamani ya 500,000/- , mshindi wa pili zawadi yenye thamani ya 300,000/-, mshindi wa tatu zawadi yenye thamani ya 200,000/-, mshindi wanne na watano zawadi zenye thamani ya 150,000/- kila mmoja, huku washiriki waliosalia watajipatia zawadi zenye thamani ya 50,000/- kila mmoja.
Zawadi hizo za fedha taslim, mali na huduma zinatolewa na wadhamini mbalimbali wakiwemo Lakairo Hotel ya Mwanza,duka la vipodozi na urembo la Happy Fashion, Duka la vifaa vya nyumbani na ofisini la BECO Business Centre, Kitemba Hotel,New Soft Saloon, studio ya picha ya kisasa ya Image for U na Duka la kisasa la Samani za ndani la Ngoto Furniture LTD la Dodoma.
Wadhamini wengine katika shindano hilo ni pamoja na NAM Hotel,Royal Village Hotel,Maezeki LTD, Dodoma Cable TV,KIU Investment, Gazeti la Jambo Leo,peter Fashion, Doble D General Traders, Globle Publishers,Magazeti ya Sanin a Clouds FM.
Imetolewa na:
Imetolewa na:
Emmanuel Msangi
Katibu Mtendaji Miss Utalii Kanda ya Kati.
No comments:
Post a Comment