Wadau waliohudhuria wakichangia hoja Mmoja wa wakilishi kutoka katika makampuni yaliyohudhuria semina ya huduma za Airtel money akichangia hoja wakati wa semina hiyo iliyozinduliwa rasmi leo na kuendesha na Mkurugenzi wa Airtel Sam Ellangallor na Mkurugenzi wa fedha Kalpesh Meltha katika ofisi za makao makuu ya Airtel.
*****************************************************************************************
Katika kuhakikisha huduma ya pesa mkononi inawafikia watanzania wengi Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Leo imeendesha semina ya huduma ya Airtel money kwa wadau na sekta mbalimbali wakiwemo wadau wa usafirishaji, asasi za kifedha, wakuu wa shule na vyuo vya elimu ya juu kwa lengo la kupambanua faida za kutumia huduma mpya ya Airtel Money katika shughuli zao zinazohusiana na maswala ya kulipa au kupokea fedha.
Akizungumza wakati wa semina iliyohudhuriwa na wadau hao na kufanyika katika makao makuu ya Airtel Tanzania Afisa Mkuu wa Biashara Walingo Chiruyi alisema "lengo la semina hii ni kutaka kujadiliana na wadau wetu faida za kuitumia huduma yetu hii mpya ya Airtel Money katika shughuli zao za kila siku.
Tumegundua huduma hii ni nyenzo muhimu sana katika kuweka urahisi usalama zaidi pamoja na kupunguza hatari zinazotokana na kutembea na fedha nyingi au kukaa ofisini na fedha nyingi kwa lengo la kuzitumia katika shughuli za wiki nzima au kulipa mahitaji mbalimbali Airtel Money ni suluhisho la kufanya hayo yote na ndio maana leo hii tumekaa pamoja kwa lengo la kuweka kila kitu bayana kwa wadau hawa muhimu kwetu!
Aliendelea kusema Bw, Akitoa maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya Airtel money ambapo kwa kupitia huduma hiyo wateja wanaweza kulipa Ankra kama vile Ada ya shule, Mishahara ya wafanyakazi au vibarua, Kufanya makusanyo ya mauzo ya siku, kulipia huduma za DSTV, Luku, bili ya Dawasco, kulipia visa ya USA, pamoja na kutuma na kupokea hela ndani na nje ya nchi.,
Aidha kwa wafanya biashara za usafirishaji huduma ya Airtel money itawasaidia katika kupunguza risk za wizi wa fedha na kuwaakikishia usalama madereva wakiwa safarini kwani malipo yote ya bidhaa baada ya usambazaji hayatafanyika tena kwa pesa taslimu bali kwa kupitia huduma ya Airtel money.
Kwa mabasi ya abiria wateja sasa wataweza kufanya booking na kulipa nauli kwa kupitia huduma ya Airtel money ambapo mteja hatakuwa na ulazima wa kutembelea kituo cha basi kukata tiketi na kulipia gharama za nauli .
Huduma ya Airtel money pia itapunguza gharama zilizopo katika kupata huduma za kifedha , na kwakupitia mtandao wetu ulioenea zaidi nchi nzima na mawaka waliosambaa kote tuna uhakika wa kuwafikia watanzania wengi zaidi walioko mjini na vijijini aliongeza Bi, Kazimoto.
Airtel hivi karibuni ilizindua na kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamefaidi kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi kwa kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hii, Huduma ya Airtel money sasa ina mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa nchi nzima hivyo ili kukamilsha upatikanaji wa huduma hii ya kisasa na rahisi zaidi . |
No comments:
Post a Comment