Tangazo

January 18, 2012

Airtel yatoa msaada wa Kompyuta katika Shule ya Sekondari Mlangarini Arumeru Arusha

Ofisa Uhusiano wa kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel,Jane Matinde akikambidhi sehemu ya msaada wa kompyuta 4, Mbunge wa Arumeru Magharibi na Naibu waziri wa Ardhi ,nyumba maendeleo na makazi Bw. Goodluck Ole Medeye kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mlangarini iliyoko Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Mlangarini iliyoko Wilayani Arumeru Mkoani Arusha,Bw. Elisa John Pallangyo akitoa maneno ya shukurani kwa kampuni ya simu ya Airtel kwa msaada mkubwa walioutoa kwa ajili ya shule hiyo,pichani kati ni mgeni rasmi wa tukio hilo, Mbunge wa Arumeru Magharibi na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Bw. Goodluck Ole Medeye ,sambamba na Diwani wa Kata ya Mlangarini, Bw.Mathias Erasto akishuhudia tukio hilo na (kushoto) ni Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde.

                                          ************************************************

 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa computer 4 kwa shule ya sekondari Mlangarini iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha ikiwa ni moja wapo kati ya shughuli za kutoa huduma zinazofanya na kampuni hiyo kwa jamii huku lengo hasa likiwa ni kukuza sekta ya elimu nchini.

 Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel, Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema, Airtel inajisikia faraja kutembelea shule ya Mlagarini na kuwapatia computer zitakazowawezesha kupata vitabu mbalimbali kwa njia ya mtandao na kutoa fulsa kwa wanafunzi wa sekondari kujifunza kutumia computer wakiwa bado mashuleni.

Aidha aliahidi kuwa Airtel itaendelea kushiriikiana na serikali kupitia wizara ya elimu katika kuhakikisha elimu mashuleni inaboreshwa.

Akiongea baada ya kukabidhiwa computer hizo Mbunge wa Arumeru Magharibi na Naibu waziri wa Ardhi Nyuma Maendeleo na Makazi Bw. Goodluck Ole Medeye alisema. "Tunashukuru sana kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuipatia shule ya sekondari Mlangarini computer zitakazowawezesha kupata habari na vitabu mbalimbali kwa njia ya mtandao, computer hizi zitarahisisha sana upatikanaji wa nyezo muhimu za elimu kwa wanafunzi na walimu kwa kupitia mtandao".

 Pia aliwaasa wanafunzi wa mlangarini kutumia fulsa hiyo kujifunza na si kutumia computer hizo kuangalia mambo yasiyofaa katika internet Ole madeye aliendelea kuwaasa na kuwapa changamoto wanafunzi kuweza kupana akili za na kuwa wavumbuzi wa vifaa muhimu zitakavyosaidia jamii kama ilivyovumbuliwa computer hiyo.

Pamoja na hayo alifafanua kuwa computer hizo zitatumika pia kwa wakazi wa maeneo hayo kwani makitaba ya wilaya itakuwa hapa shuleni hivyo basi wakazi wa wilaya ya Arumeru watapata fulsa ya kutangaza biashara zao kwa kupitia mtandao na kuweza kupata taarifa muhimu zitakazo wasaidia katika kuboresha biashara zao na shughuli muhimu za wilayani hapo pia aliongeza Madeye.

 Naye Diwani wa kata ya Arumeru Bw Martias Manga alichukua fulsa pia kuwashukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kuwaasa wanafunzi kutumia computer hizo vizuri na kuzitunza ili zisaidie wanafunzi wengi zaidi shule hapo. Aliwaasa wanafunzi hao kuchukua nafasi hii ya pekee kujifunza na kutumia computer hizo katika kujijenga kielimu na kitaaluma zaidi.

 Akitoa shukurani Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elisa John Pallangyo ameipongeza Airtel kwa kuwafikishia msaada muhimu shuleni hapo na kuahidi kwa kupitia msaada kiwango cha elimu shuleni hapa kitapanda kwani changamoto mbalimbali walizokuwa nazo kama vile internet, upatikanaji wa nyenzo muhimu katika kufundishia zitapungua kwa kiasi kikubwa sana.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, kuchangia katika huduma za afya ambapo wiki iliyoopita waligawa baskeli kumi katika vituo vya afya wilayani misungwi na kutoa mchango wao pia katika sekta ya michezo kwa kudhamini michezo mbalimbali nchini.

No comments: