Tangazo

January 26, 2012

Mbunge Mstaafu wa Kalenga, Stephen Jones Galinoma afariki Dunia

 Marehemu Stephen Jones Galinoma
Habari za uhakika  kutoka Kalenga katika Wilaya ya Iringa Vijijini zinasema kuwa Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kalenga,  Mhe.Stephen Jones Galinoma (pichani)  amefariki dunia asubuhi hii wakati akikimbizwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Iringa  ya Ipamba .

Habari ambazo mtandao huu umezipata na kuthibitishiwa na Mtoto wa marehemu, Bi.  Magreth zinadai kuwa Galinoma amefariki majira ya asubuhi ya leo wakati akikimbizwa hospital hiyo ya Ipamba .

Alisema kuwa marehemu kabla ya kifo chake alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo na taarifa zaidi utaendelea kuzipata katika mtandao huu .

Marehemu Galinoma alikuwa mbunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 alipostaafu na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa sasa, Dk. Wiliam Mgimwa .
                                  Mungu amlaze mahala pema peponi.

Kwa habari zaidi za msiba wasiliana na:

Joseph Galinoma kwa namba hii 00255716492048 au Denis Galinoma namba hii 00255784769945


No comments: