Tangazo

January 29, 2012

MSD yaipiga jeki Twiga Stars


Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah hundi yenye thamani ya sh. mil. 10 ikiwa ni msaada kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia. Katika mechi hiyo ya marudiano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake iliyochezwa leo Januari 29. Twiga Stars imeikung'uta Namibia mabao 5-2.

Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo (kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah wakiwa na furaha wakati wa hafla ya MSD, kukabidhi  msaada wa Sh. Mil. 10  kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, Dar es Salaam jana.

Katibu Mkuu TFF, Angetile Osiah (kushoto) akitoa shukurani kwa MSD kuipatia timu hiyo msaada. Katikati ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo.

Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia (kushoto), akielezea umuhimu wa msaada huo kwa timu hiyo ya soka kwa wanawake. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah.

No comments: