Tangazo

January 20, 2012

Watu 6 wauawa mjini Mogadishu.

Mlipuko wa bomu mjini Mogadishu.
Mlipuko wa Bomu umetokea ndani ya kambi iliyofurika katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, muda mfupi baada ya kundi la maafisa wa Umoja wa Mataifa kuondoka mahali hapo.

Takriban watu sita wamefariki na inahofiwa idadi hiyo ikaongezeka kwani watu wengi zaidi wamejeruhiwa.

Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa na waandishi wa Habari wa kimataifa kuzuru eneo hilo.

Mwandishi wa BBC Odhiambo Joseph alikuwa miongoni mwa waandishi wa habari kwenye msafara wa Umoja wa Mataifa, uliokuwa ukikagua oparesheni za utoaji misaada na akashuhudia mlipuko huo.

Shirika la kimataifa la kutoa misaada la Medicine Sans Frontiers limesema kuwa limefunga vituo vyake viwili vya matibabu katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadisu, kufuatia kuuawa kwa wafanyakaza wake wawili.

Wawili hao waliuawa mwezi uliopita na mmoja wao alikuwa raia wa Ubelgiji na mwingine kutoka Indonesia.

kufuatia uamuzi huo shughuli za shirika hilo mjini Mogadishu zimepunguzwa kwa asilimia 50.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Christopher Stokes amesema ni vigumu kusitisha huduma muhimu katika eneo ambalo huduma hizo zilihitajika ili kuokoa maisha ya raia.

Kufuatia mauaji hayo imekuwa vigumu kwa shirika hilo kuendelea kuhudumu katika wilaya hiyo ambayo mauaji hayo yalitokea.
 

No comments: