Tangazo

February 6, 2012

AIRTEL yatoa vitabu kwa Shule Nne za Sekondari Mkoani Manyara


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Yaeda Ampa,  Mary Genda  na wanafunzi  wa shule hiyo wakipokea vitabu toka kwa Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule za sekondari nne za mkoa wa Manyara ambazo ni  Yaeda Ampa, Yaeda Chii , Naberera na Merelani B.W. Mkapa chini ya mpango wake wa shule yetu. Halfa ya makabidhiano ilifanyika mwishoni mwa wiki hii.


Afisa Uhusiano wa Airtel ,Jane Matinde akikabidhi  vitabu kwa Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Mbulu, Mikaeli Hadu  kwa niaba ya shule nne za sekondari zilizokabidhiwa vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kila shuke, shule hizo ni  Yaeda Ampa, Yaeda Chii , Naberera na Merelani B.W. Mkapa,  Mkoani Manyara. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Bw.Harry Sinjela.

Wanafunzi , walimu ,wafanyakazi wa Airtel na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Airtel kukabidhi vitabu hivyo.

No comments: