Tangazo

February 3, 2012

Bondia 'Prince Naseem' kutetea Ubingwa wake Februari 24

Kocha wa mchezo wa ngumi Saba Joseph (kulia) akimwelekeza bondia Saleh Mkalekwa jinsi ya kutupa masumbwi katika kambi yake iliyopo Mbagala Mkalekwa anajihandaa na mpambano wa ubingwa wa PST dhidi ya Abdalah Mohamed 'Prince Naseem' Februari 24. Picha zote kwa jhisani ya superdboxingcoach.blogspot.com



Bondia Saleh Mkalekwa akijifua kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa ubingwa wa PST na  Abdalah Mohamed 'Prince Naseem' Februari 24.

Bondia Abdallah Mohamed 'Prince Nassim' (kulia) akifuliwa na kocha wake msaidizi Rajabu Rashidi wakati wa mazoezi yanayoendelea ufukwe wa ufukwe wa Mtoni Kijichi kwa ajili ya kutetea ubingwa wake dhidi ya bondia Saleh Mkalekwa Februari 24.
                     **********************************************************************************


Na Mwandishi Wetu

BINGWA wa mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Abdalah Mohamed 'Prince Naseem' atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa PST Februari 24 mwaka huu dhidi ya Salehe Mkalekwa.

Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa ni pambano la uzito wa kg 57 na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Shaban Adiosi 'Mwayamwaya' alisema pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa New Kibeta uliopo mbagala kuu Dar es Salaam.

Alisema pambano hilo la ubingwa wa PST ni muendelezo wa shirikisho hilo kuendelea kuwainua mabondia chipkizi ambao hawajawa na majina makubwa ili nao waweze kufikia kiwango kizuri cha mchezo huo.

"Ubingwa huu wa PST ni maalum kwa ajili ya mabondia chipukizi na ndio maana mabondia wanaoshirikishwa wengi ni chipkizi na lengo ni kuendeleza vipaji vyao,"alisema Mwayamwaya.

Aliyataja mapambano ya utangulizi yatakayopamba pambano hilo yatakuwa kati ya Shaaban Zungu na Hasan Salehe watakaopigana uzito wa kg 55, Safari Mbeyu na Ibrahim Maokola watakaopigana uzito wa kg 67, Jofrey Pacho atakayetwangana na Seleman Shaaban na Abdalah Yusuph atakayepigana na Omari Kijepa.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.

“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

No comments: