Tangazo

February 22, 2012

PSPF yatoa Msaada wa Madawati katika Shule ya Msingi Bwilingu - Chalinze Pwani

Kaimu Mkurugenzi Ukaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Pensheni wa Utumishi wa Umma (PSPF), Bw. Godfrey Ngonyani (kulia) akizungumza na Wazazi na Wanafunzi pamoja na Bodi ya Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani wakati walipokwenda kukabidhi msaada wa Madawati 60 yenye thamani ya milioni tatu.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Bi. Anifa Kombo na Mjumbe wa Bodi ya PSPF Bw. Ramadhani Maneno.(Picha na Mpigapicha Wetu)

Kaimu Mkurugenzi Ukaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Pensheni wa Utumishi wa Umma (PSPF), Bw. Godfrey Ngonyani (kushoto) akikabidhi msaada wa Madawati 60 yenye thamani ya milioni tatu walioutoa leo kwa Mjumbe wa Kamati ya Shule Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani, Bi. Jacklin Kitego (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Anifa Kombo.(Picha na Mpigapicha Wetu)

Baadhi ya Wanafunzi wa  Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani wakigombania kukaa kwenye madawati mapya 60 yenye thamani ya Milioni 3/- walioletewa na Mfuko wa Pensheni wa Utumishi wa Umma PSPF.(Picha na Mpigapicha Wetu)

No comments: