Tangazo

February 7, 2012

RAIS JAKAYA NA MAKAMU WAKE WASHUHUDIA ZOEZI LA UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA KUDHIBITI MAHARAMIA (MoU) KATI YA TANZANIA, MSUMBIJI NA AFRIKA YA KUSINI, IKULU LEO

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal (nyuma) wakishuhudia zoezi la utiaji saini wakati Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Husein Mwinyi, akisaini mkataba wa makubaliano (MoU) ya Ushirikiano katika mapambano dhidi ya Maharamia kati ya Tanzania, Afrika ya Kusini na Msumbiji, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Februari 7, 2012. Kushoto ni Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi na (kulia) ni Waziri wa Ulinzi wa Afrika ya Kusni, Lindiwe Sisulu. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Rais Jakaya Kikwete na  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakishuhudia Waziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto)na  wa Tanzania  Dr Hussein Mwinyi  wakibadilishana nyaraka huku  wa Afrika Kusini  DKT L.N. Sisulu akitazama baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.Picha/Ikulu

Rais Jakaya Kikwete akiongea baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.Picha/Ikulu

Rais Jakaya Kikwete na  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiongea na Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Tanzania  Dr Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), na wa Afrika Kusini  DKT L.N. Sisulu baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao. Picha/Ikulu

No comments: