XXXXXXXXXXXXXX
Arusha
Kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya ngozi,uharibifu wa macho maarufu kwa jina la mtoto wa jicho, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi, kumeelezwa kuwa husababishwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa tabaka la ozone ambapo kunatokana na shughuli za kibinadamu kama vile matumizi ya kemikali haribifu na zisizo rafiki kwa mazingira.

Hayo yameelezwa leo Mjini Arusha katika hotuba ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya mafundi mchundo wa majokofu na viyoyozi kuhusu teknolojia mbadala ya majokofu na viyoyozi, iliyosomwa na Afisa Mazingira wa Mkoa bw.Julius Achiula kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa.
Akisoma hotuba hiyo,Bw. Achiula ameainisha baadhi ya chemikali hizo kuwa ni methyl bromide, halons na chloroflorocarborns ambazo hutumika kama vipozi katika mafriji, viyoyozi, vifaa vya kuzima moto, usafishaaji chuma, ufikizaji wa mazao katika maghala na utengenezaji wa magodoro ambazo huleta madhara kwa tabaka la ozone na adhari zake hotokea kwa binadamu, mimea na viumbe hai.
Uhifadhi wa tabaka la ozone umetokana na utekelezaji wa Mkataba wa Montreal na Vienna ambayo Tanzania ni mwanachama.
Warsha hiyo inayoratibiwa na Ofisi ya makamu wa rais imehusisha washiriki kutoka, baraza la taifa la Hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC, chuo cha ufundi VETA Moshi, wanahabari, maafisa mazingira wa mkoa wa arusha na mafundi mchundo.
Imetolewa na: Evelyn Mkokoi Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment