Tangazo

April 18, 2012

Vodacom Tanzania yashinda Tuzo ya Uwekezaji katika Jamii

Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo kwa Wateja wakubwa wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba akifurahia tuzo ya Uwekezaji Endelevu katika Jamii Afrika Mashariki inayotolewa na Bank M mara baada ya kuipokea kutoka kwa Balozi wa Burundi nchini Issa Ntambuka(Kulia). Vodacom Tanzania imeshinda tuzo hiyo kupitia mradi wake wa kusaidia wajasiriamali wadogo wanawake uitwao MWEI. Kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation katika masuala ya ustawi wa jamii Mwamvua Mlangwa anaeusimamia mradi huo.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt akisoma tuzo ya Uwekezaji Bora Endelevu katika Jamii kwa Makampuni ya Afrika Mashariki iliyotunukiwa kampuni ya Vodacom Tanzania kutokana na mradi wake wa kusaidia wajasiriamali wadogo wanawake vijijini wa MWEI. Kulia ni Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo kwa Wateja Wakubwa Mwamvita Makamba.Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika jana usiku jijini Dar es salaam.

Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo kwa Wateja Wakubwa wa Vodacom Tanzania,Mwamvita Makamba akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo ya  Uwekezaji Endelevu katika Jamii Afrika Mashariki wakati wa utoji wa Tuzo hizo inayotolewa na Bank M kwa makampuni  bora ya Afrika Mashariki. Vodacom Tanzania imeshinda tuzo hiyo kupitia mradi wake wa kusaidia wajasiriamali wadogo vijijini wa MWEI. Kulia ni Meneja  wa mradi huo Mwamvua Mlangwa.Hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es salaam.



No comments: