Tangazo

May 22, 2012

WAREMBO WA MISS DAR INTER COLLEGE KUINGIA KAMBINI LEO: Rose John kuwanoa

Mratibu , Dina Ismail
 Na Vicky Kombe

WAREMBO watakaoshiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 leo wanatarajiwa kuanza mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo kwenye hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo, Dina Ismail alisema kwamba warembo hao watatoka katika vyuo vya  Elimu ya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ), TIME pamoja na  Ustawi wa Jamii.
Rose John

“Kesho (leo) tutaanza mazoezi yetu pale Lamada ambapo warembo kutoka vyuo vinne wataanza kujinoa…wiki ijayo huenda tukaongeza washiriki wengine ambao watatoa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambao wanafanya shindano lao mwishoni mwa wiki hii”, alisema.

 Alisema kuwa warembo hao watakuwa chini ya ukufunzi wa mrembo aliyepata kushiriki shindano hilo, Rose John huku kwa upande wa shoo watanolewa na Bob Rich.

 Dina aliwataja wadhamini waliojitokeza mpaka sasa ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, na  Dodoma Wine, huku akiomba makampuni mengine kujitokeza kudhamini shindano hilo litakalofanyika mwezi ujao.

No comments: