Tangazo

May 22, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA KITABU CHA ‘CHECKLIST OF TANZANIAN SPECIES’

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’ wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Mei 22, 2012. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dkt. Hassan Mshinda. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’ baada ya  kukizindua rasmi kitabu hicho wakati wa hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Mei 22, 2012. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dkt. Hassan Mshinda. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Baadhi ya wadau waliohudhulia uzinduzi huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Meneja wa Shirika la TANBIF Node, Hulda Gideon, wakati alipotembelea sehemu ya maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika hilo kwenye uzinduzi wa Kitabu cha ‘Checklist Of Tanzanian Species’ uliofanyika leo Mei 22, 2012 jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika Picha ya pamoja na wadau waliohudhuria uzinduzi huo.

No comments: