Tangazo

June 1, 2012

Airtel yatoa burudani kwa kudhamini onesho la muziki wa Classic.

Kikundi cha muziki wa taratibu (classic) cha Dar Choral Society kikitoa burudani katika onyesho la muziki huo lililodhaminiwa na Airtel katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.

 Meneja Huduma wa Airtel, Hilda Nakajumo akitoa maelezo kwa  Mkuu wa Biashara wa Benki ya Africa, Wasia Mushi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel  katika onyesho kikundi cha Dar Choral Society lililodhaminiwa na Airtel katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya watu wakiohudhuria onyesho hilo wakipata maelezo ya huduma zitolewazo na Airtel katika eneo lililowekwa ambapo huduma mbalimbali zilipatikana.

Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Tanzania, Irene Madeje Mlola (kushoto) akizungumza na baadhi ya watu  waliohudhuria onyesho la kikundi cha muziki cha  Dar Choral Society lililodhaminiwa na Airtel katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam jana. Picha na Father Kidevu

No comments: