Tangazo

June 12, 2012

BMT yamuaga Dk. Nchimbi na Kumkaribisha Dk. Mukangara Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi akihutubia wakati wa hafla iliyoandaliwa na BMT kwa ajili ya kumuaga rasmi aliyekuwa waziri katika wizara hiyo, Dk. Nchimbi iliyofanyika katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam Juni 10.2012. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Waziri wa zamani wa wizara hiyo ambaye kwa sasa ni  Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wageni waalikwa ambao ni viongozi mbalimbali wa vyama vya michezo.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akihutubia hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi akikabidhi zawadi kwa Dk. Emmanuel Nchimbi.

Wasanii wa kikundi cha Afro Dance wakitumbuiza.

Msanii wa Kikundi cha Afro Dance, Deborah Dickson akionyesha kipaji chake.

Kutoka Kushoto: Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakingua zawadi za Simu za mkononi walizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi (kulia) wakati wa hafla iliyoandaliwa na BMT kwa ajili ya kumuaga rasmi aliyekuwa waziri katika wizara hiyo, Dk. Nchimbi.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi akikabidhi zawadi kwa Amos Makala.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi akikabidhi zawadi kwa Dk. Fenella Mukangara.

Kutoka Kushoto: Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakifurahia zawadi za Simu za mkononi walizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi (kulia) wakati wa hafla iliyoandaliwa na BMT kwa ajili ya kumuaga rasmi aliyekuwa waziri katika wizara hiyo, Dk. Nchimbi.

Rais wa TFF, Sir Leodger Tenga akikabidhi tuzo kwa Dk. Nchimbi kutokana na  mchango wake mkubwa katika maendeleo ya soka hapa nchini wakati akiwa Waziri wa Michezo. Kulia ni Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi.

Tanzania Golf Union (TGU), nao walitoa zawadi ya kinyago. Kulia ni Foti Gwebe wa TGU

Wakati wa misosi uliwadia.

Nyama choma za kumwaga.


JKT Still Band wakitumbuiza.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Zuwena Iddi Kipingu (fulana nyekundu), akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga (kulia kwake).

Mwenyekiti wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Zuwena Iddi Kipingu akisalimiana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara

No comments: