Baadhi ya
waandishi wa habari wakijaribu kutafuta ishara za madini ya almasi Mji mdogo wa
Songwa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga yalipo machimbo ya almasi
"
Baadhi ya
waandishi wa habari hao wakipiga picha na baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliofanya mahojiano
mbalimbali na wanahabari."Baadhi ya waandishi wa habari hao wakipiga picha na baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliofanya mahojiano mbalimbali na wanahabari."
Hapa tukipata
picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari wa mkoani Shinyanga katika ofisi yao ya mkoa.
"Waandishi
wanaofanya habari za uchunguzi maeneo ya vijijini Kata ya Songwa, Wilaya ya
Kishapu mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza
warsha ya siku mbili iliyoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)
kabla ya kuingia kazini."[/
Na Mwandishi wa Thehabari.com,
Songwa-Shinyanga
BAADHI ya waandishi kutoka jijini Dar es
Salaam na mkoani Shinyanga wametembelea machimbo ya almasi yanayofanywa na
wananchi eneo la mjini mdogo wa Songwa.
Ziara ya waandishi hao imekwenda sambamba na kufanya
uchunguzi juu ya huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa na Serikali kwa
wakazi wa maeneo hayo, yaliomo ndani ya Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga.
Waandishi hao wameshuhudia namna wananchi na hasa vijana
wanavyojishughulisha na shughuli nzima za machimbo ya madini ya almasi licha ya
Kata ya Songwe kukabiliwa na huduma duni za maji safi na salama kwa matumizi
yao pamoja na yale ya shughuli za machimbo.
Mtandao huu utawaletea mahojiano ya wananchi eneo hilo pamoja na hali
halisi ya huduma anuai za kijamii kwa wakazi wa Kata hiyo ya Songwa iliyopo
Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga muda si mrefu.
No comments:
Post a Comment