Tangazo

June 5, 2012

Watanzania Msaidieni Mhariri wa Picha wa Magazeti ya Serikali (TSN), Athuman Hamis



Mhariri wa Picha wa Habari Leo  gazeti linalochapishwa na Tanzania Standard Newspaper (TSN), athuman Hamis  akizungumza na waandishi wa habari juu mustakabali wa maisha yake tokea amepata ajali ya gari. Athuman ambaye alipata ajali ya gari Septemba 12.2008 katika eneo la Kibiti mkoani Pwani na kupelekea kuvunjika shingo na kudamage spinal cord hali inaliyopelekea kupooza mwili mzima hivi sasa yuko katika hali ngumu ya kimaisha ambapo anahitaji wasamaria wema kumsaidia ili aweze kukabiliana na ukali wa maisha.

Akisisitiza kwa Mapaparazi Bw. Athuman Alisema, "Nimekuja leo kuutangazia Umma hali ilivyo. Ukweli kwa sasa Akaunti yangu ya CRDB ilikuwa maalum kwa ajili ya kusomeshea watoto, imekauka na ile ya Benki ya Posta ambayo ilikuwa ni kwajili ya mshahara haina kitu. Pesa ya mshahara inayoingia benki kutoka kwa mwajiri wangu ni  450,000/- tu.

Aidha akafafanua zaidi kuwa anamlipa Nurse wake, Bi. Elizabeth Richard  (kulia pichani) na Msaidizi wake na Mfanyakazi kiasi cha 370,000/- na pia ana watoto watatu,  wa kwanza anamaliza Darasa la Saba Mwaka huu, wa Pili yuko la Darasa Nne na wa Mwisho huko Darasa la Pili.

Hawa wanaosoma shule ya msingi niza kulipia 200,000/- kula term jumla 400,000/- hizo shule zina term nne kila mwaka. Gharama chakula, vifaa vya wanafunzi, gharama zao ndogo ndogo na za kifamilia pamoja na chakula kwa mwezi, inakwenda kati ya 750,000/- mpaka 900,000/- kwa mwezi.

"Nimekuwa omba omba mpaka watu kadhaa siwalaumu, wamechoka hawapokei simu zangu wala kujibu SMS. Siyo siri, ndugu wote wamekimbia waliobaki ni marafiki wa kweli wamenitangazia katika familia zao. Hali yangu ni mbaya sana kiuchumi", aliongea kwa uchungu.

Sina uwezo wa kulipia nyumba kwa gharama zozote zile. Mimi Athuman Hamisi naomba watanzania watakaoguswa wanisaidie. Kubwa nyumba na ushauri wa madaktari walionishauri nisiishi mbali na mazingira ya hospitali kulingana na hali yangu.

KWA YEYOTE ALIYEGUSWA NA MATATIZO YA BW. ATHUMAN HAMIS ANAWEZA KUMSAIDIA  KWA MAWASILIANO HAYA CHINI; 
 
Makampuni, Mshirika, Wizara yoyote, Shirika la Nyumba la Taifa NHC, Watu binafsi, Serikali na Taasisi yoyote watakaoguswa na kilio changu nawaomba wanisaidie kwa nia yoyote. Kwa walio tayari naomba misaada ipitie katika account ya CRDB no; 01J2027048800 na Account ya Postal Benki no; 010-00090488.

Kwa wanaotumia mitandao ya simu wanaweza kutumia M-Pesa 0757825737, Tigo Pesa 0655531188 na Airtel Money 0784531188. Au unaweza kumtumia rafiki yake Bw. Chris Mahundi M-Pesa 0767298888, Ephraim Mafuru Airtel Money 0686710977.

NB:
Athuman kwa sasa emepewa Notice katika nyumba aliyokuwa anaishi katika eneo la Sinza ambapo awali nyumba hiyo ilikuwa ikilipiwa na mwajiri wake TSN, lakini kwa sasa inaonekana mwajiri wake hana mpango wa kumlipia tena.

Daily Mitikasi Blog inawaomba watu wote wenye moyo kujitolea ndani na nje ya nchi yetu kumsadia ndugu yetu Athuman.



No comments: