Tangazo

July 3, 2012

BIA YA NDOVU SPECIAL MALT NDANI YA MUONEKANO MPYA WENYE MVUTO ZAIDI

Meneja wa Bia ya Ndovu, Pamela Kikuli.

Bia ya Ndovu katika muonekano mpya.

Meneja wa Bia ya Ndovu, Pamela Kikuli akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa bia hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Habari wa TBL, Edith Mushi.

*****************************
 Bia ya Ndovu Special Malt inayotengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), imezindua muonekano wake mpya ambao umeiongezea bia hiyo yenye hadhi ya juu hapa nchini na kimataifa mvuto zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam, meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema; Tunayo furaha kubwa sana siku ya leo kuzindua muonekano mpya wa Bia hii ya Ndovu Special Malt. Lengo kuu la maboresho haya yaliyofanyika ni kuipa Bia hii ya Ndovu muonekano wenye mvuto zaidi, lakini pia kuvipa muonekano zaidi vitu muhimu vinavyoitambulisha bia hii.

Ukiangalia katika lebo ya mbele, picha ya mnyama Tembo, au kwa jina jingine Ndovu imeongezwa ukubwa, hii ni kwa sababu maalum za kumpa uzito unaostahili mnyama huyu ambae ndio kitambulisho namba moja cha bia hii.

Maboresho mengine yaliyofanywa ni pamoja na kuboresha nembo ya kiungo muhimu kinachoitofautisha bia ya Ndovu na bia nyingine “Cristal Malt”, pia lebo inayozunguka shingo ya bia hii (foil) ambayo sasa ina mg’ao angavu wa dhahabu. Wapenzi wa Bia hii ya Ndovu special Malt watapata pia historia ya bia hii katika lebo ya nyuma hivyo kuwawezesha kuielewa bia yao vizuri zaidi. Tunatarajia maboresho haya yatawavutia zaidi wadau wa Ndovu Special Malt na hivyo kuongeza mafanikio ya bia hii. Alisema Pamela.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano na Habari wa TBL Bi. Edith Mushi alisema; Bia hii ya Ndovu Special Malt, imeendelea na itaendelea kuongoza katika ubora wa Bia za Kitanzania katika soko la ndani na nje pia. Hii inatokana na umakini unaotumika katika kutengeneza bia hii, ikiwemo kiungo cha “Cristal Malt” kinachoitofautisha na kuifanya bia hii iwe juu ya bia zote hapa nchini.

Yote haya yanathibitishwa na ushindi mkubwa na wa kishindo ambao Bia hii imekuwa ikijitwalia katika tuzo za kimataifa kutokana na ubora wake. Mwaka huu kwa mara nyingine tena Bia hii ya Ndovu Special Malt imeshinda tuzo yenye hadhi ya juu kabisa ya bidhaa za kimataifa kwa mara ya pili.

Tuzo hizi  hutolewa na Taasisi ya kimataifa inayoangalia ubora wa bidhaa ya “Monde Selection International Quality Institute” iliyopo Athens, Ugiriki.

Tuzo hii inajulikana kama “Grand Gold Quality  Award” na hushindanisha bidhaa toka Mataifa mbalimbali. Hivyo hii inawathibitishia wadau wote wa bia hii kuwa wanafanya uchaguzi na maamuzi sahihi kwa kuchagua kutumia Ndovu Special Malt, kwani ubora wake unajidhihirisha kimataifa.

No comments: