MUHIMBILI
NATIONAL HOSPITAL
|
Cables: "MUHIMBILI"
Postal Address:
Telephones: 255-22-2151367-9 P.O. BOX 65000
Fax: 255-22-2150234 DAR ES SALAAM
MADAKTARI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI WAREJEA KAZINI
JULAI 2, 2012
Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya
leo Julai 2, 2012.
Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili
hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari
Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki
zote za tiba zimefanyika kama kawaida.
Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini
wengine wawili wako likizo na Registrar
watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo
Upande wa OPD yenye Registrars
saba, sita kati yao
walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja
kazini.
Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri
Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.
Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.
Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za
huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani
hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji..
KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.
Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 2, 2012
No comments:
Post a Comment