Twanga Pepeta |
Msondo Ngoma |
BENDI zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Siboka walioandaa tamasha hilo, alisema siku hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza na kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo, pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema Siboka.
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo nbalo litapambwa na sherehe mbalimbali.
Siboka pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni pamoja naTBL kupitia bia za Safari na Kilimanjaro, SBC Tanzania (Pepsi), Dstv n mengine mengi.
No comments:
Post a Comment