Wachezaji wa Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakishangilia ubingwa wao wakiwa na Kombe la Kagame baada ya kukabidhiwa rasmi walipoibanjua timu ya Azam Fc kwa mabao 2-0, katika mchezo wa Fainali uliozikutanisha timu hizo katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jana jioni.
*****************************
TIMU ya Yanga ya jijini ya Dar es Salaam, leo imewadhihirishia mashabiki wa soka kwa kutetea ubingwa wake na kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame 2012,katika mchezo wa Fainali za Kombe hilo dhidi yake na timu ya wauza Lambalamba Azam Fc, na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Taifa.

Yanga sasa imebakiza mara moja kufikisha idadi sawa na wapinzani wao wa jadi, Simba kutwaa Kombe hilo, mara tano kwa sita. Yanga ilibeba taji hilo 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Hamisi Kiiza aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 44 na Said Bahanuzi aliyefunga la pili dakika ya 90+ katika dakika tatu za nyongeza.
Kiiza alifunga bao lake, baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na kipa Deo Munishi ‘Dida’ na kumpiga chenga kipa huyo kisha kuusukuma mpira nyavuni.
Bahanuzi aliuwahi mpira mrefu uliopigwa na beki Oscar Joshua na kuwazidi ujanja mabeki wa Azam kabla ya kumtungua Dida.
No comments:
Post a Comment