Tangazo

August 9, 2012

BENKI YA KIISLAM YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ) WAFUTURU NA MAKAMU WA RAIS DK. BILAL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongazana  na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana Agosti 8, 2012 kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo na kufutari pamoja na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati wa  hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu  pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo, jana Agosti 8, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

 Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, akizungumza machache kuhusu kazi na utendaji wa kazi za Benki hiyo ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na malengo yake wakati wa hafla hiyo ya futari  iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

 Akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.


Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakipata futari wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakishiriki kuomba dua ya pamoja  wakati wa hafla hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana Agosti 8, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) jana, Agosti 8, 2012 katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh, Abdulla Tarib Abdulla  na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) jana katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: