Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amemwapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama pamoja na Msajili mkuu wa Mahakama na msajili wa mahakama ya rufani katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam. Walioapishwa leo ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bwana Hussein Katanga, Msajili Mkuu wa Mahakama, Bw. Ignus Paul Kitusi na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Bw. Panterine Muliisa Kente. PICHANI: Mtendaji mkuu wa Mahakama, Bw. Hussein Katanga akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. |
No comments:
Post a Comment