Tangazo

September 5, 2012

TBL 'yamwaga' Vifaa vya Michezo kwa Klabu za Yanga na Simba

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Louis Sendeu (kushoto) na akamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' , ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji hicho kwa Klabu za Simba na Yanga, katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ya TFF, jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kulia) ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba. PICHA ZOTE/DAILY MITIKASI BLOG

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'. Anayeshudia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (katikati), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Louis Sendeu. Kulia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Louis Sendeu (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' (kulia) wakionyesha kwa waandishi wa habari baadhi ya vifaa vya michezo baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (wa pili kushoto), ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji hicho kwa Klabu za Simba na Yanga, katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ya TFF, jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kulia) ni na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.

No comments: