Tangazo

October 19, 2012

Sheikh Issa Ponda na wenzake 50 waburuzwa Kortini


Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Sheikh Issa Ponda (katikati) akiwa na wenzake 50 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mapema jana, walipofika kusomewa mashtaka ya makosa yao mbali mbali yakiwemo ya uchochezi wa kidini.

Ponda na wenzake walipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo kujibu mashtaka mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashawishi baadhi ya Waislamu kuvamia  Kiwanja katika eneo la Chang'ombe jijini Dar es Salaam, kuwashawishi Waislamu kutojitokeza katika zoezi la Uandikishaji katika Sensa ya Watu na Makazi.

No comments: