Tangazo

October 29, 2012

Twiga Cement yakabidhi zawadi kwa washindi wa Tuzo za Mazingira

Mkurugenzi Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto) akimpongeza  Leonard Gastory Lugali, akiyeibuka mshindi wa kwanza wa shindano kuhusu  mazingira lililopewa jina la‘Quarry Life Award’ lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Saruji yaTanzania Portland Cement (Twiga) na kupewa zawadi ya EURO 5000 katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo, Dar es Salaam leo. Mshindi wa pili alipewa EURO 5000 na wa tatu aliondoka na 1500. Wengine pichani washindi, majaji wa shindano na maofisa wa TPCC.

Mkurugenzi Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Euro 3000 kwa David Dawson Maleko, akiyeibuka mshindi wa pili wa shindano kuhusu  mazingira lililopewa jina la ‘Quarry Life Award’ lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Saruji ya Tanzania Portland Cement (Twiga) katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo, Dar es Salaam leo.  Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa TPCC, Ignatius Asare, , Ofisa Mazingira, David Mwakalobo, Meneja Mazingira wa Twiga, Juliet Mboneko Tibaijuka  na Meneja Mazingira kutoka HeidelbergCement, Dk Michael Rademacher.

Mkurugenzi Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto) akikabidhi cheti kwa Meneja Mazingira wa TPCC, Juliet Mboneko Tibaijuka, mmoja wa watu waliofanikisha mchakato wa tuzo hizo.


Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe za kukabidhi tuzo kwa washindi wa shindano la mazingira lililoandaliwa na Twiga Cement jijini Dar es Salaam leo.

No comments: