Tangazo

November 5, 2012

MABINGWA WA BALIMI BOAT RACE MWANZA WAPATIKANA

 Wapiga makasia 15 wakinyosha makasia yao juu kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika jijini Mwanza jana.

Mabingwa wa ngoma za asili wa mashindano ya ngoma ya kanda ya ziwa kikundi cha Bujora wakitumbuiza mashabiki wa mashindano ya mitumbwi yaliyofanyika jana kwenye fukwe za Mwaloni Mkoani Mwanza jana ambapo washindi watakaowakilisha mkoa huo kwenye fainali wamepatikana.
 

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akiteta jambo na Afisa Utamaduni na Michezo wa Manispaa ya Ilemela wakati wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika jana Mkoani Mwanza.
 
Msanii wa kikundi cha ngoma cha Bujora akichezea nyoka kwa kuingiza kichwa mdomoni wakati wakitumbuiza watu waliofika kushuhudia mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika Mwaloni Mkoani Mwanza jana.

Mabingwa wa Mkoa wa Mwanza wa Mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) timu ya Cheka na Wengi kutoka Misungwi wakiwasili ufukweni baada ya kuongoza mbio hizo muda wote huku wanaofuatia wakipishana kwa sekunde tu.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL Fimbo Butallah, akimuelekeza jambo Nahodha wa timu ya Wanawake na Maendeleo ya Misungwi Tabu Daudi, ambao ndio washindi wa kwanza  kwa upande wa wanawake Mkoa wa Mwanza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yao ya ushindi wa kwanza kitita cha shilingi laki saba (700,000).

Mashabiki waliohudhuria.

No comments: