***************************
· Airtel yachangia vitabu vya sayansi kwa shule tatu za Sekondari mkoani Mwanza
Wakati Tanzania ikikabiliwa na uhaba wa wataalamu wa fani ya sayansi,wanafunzi wametakiwa kutohofia masomo ya sayansi na kukimbilia kusoma masomo mengine kwa lengo la kulifanya taifa liwe na wataalamu wengi wa fani mbalimbali.Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza Hamis Maulid wakati akikabidhi vitabu kwa shule nne za sekondari za mkoa huo vilivyotelewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
Afisa Elimu wa mkoa wa mwanza ameendelea kwa kusema elimu ni urithi endelevu na kusoma masomo ya sayansi kunamwezesha mwanafunzi kuwa katika nafasi nzuri ya kulisaidia taifa katika Nyanja ya kitaalamu. mataifa mengi duniani yamepiga hatua kutokana na wanafunzi kupewa msukumo wa kusoma masomo ya mchepuo wa sayansi.
Akiongea katika halfa ya makabithiano ya vitabu mkoani Mwanza, Meneja wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Hawa Bayumi amesema Airtel imeguswa na tatizo la ukosefu wa vitabu mashuleni na kusababisha kiwango cha ufaulu kushuka hasa katika masomo ya sayansi. Na leo tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari za mkoa wa mwanza zikiwemo: Kalebezo sekondari iliyopo wilayani Sengerema, shule ya sekondari ya Buhongwa na Kabuhoro sekondari.
Tunaamini mchango huu wa vitabu mashule utakuwa chachu ya maendeleo ya elimu nchini na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini. Tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunafikia malengo waliojiwekea. Aliongeza Bayumi.
Naye Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kalebezo iliyopo wilayani Sengerema Thomas Muswaga na mwanafuzi Julieth John wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Buhongwa wanazungumzia changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa vitabu na kushukuru Airtel kwa msaada wa vitabu walioutoa katika shule hizo za mkoa wa Mwanza.
Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu imeendelea kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari mbalimbali nchini. kwa mwaka huu shule 93 za sekondari tangu kuanzishwa kwa mradi huo shule zaidi ya shule za sekondari 900 zimekabithiwa.
No comments:
Post a Comment