Tangazo

February 21, 2013

Peter Amandus ajishindia Milioni 5/- za DStv Rewards

Mfanyakazi wa TRA, Peter Amandus (wa pili kulia) akifurahia Tshs 5,000,000 baada ya kuzawadiwa na DStv kwa kulipia akaunti yake ya DStv kabla ya kukatika. Kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi, Meneja Uendeshaji, Ronald Shelukindo (wa pili kushoto) na Meneja Masoko, Furaha Samalu.

**************************
Mshindi wa kwanza wa Milioni 5/- kwanza katika kampeni ya DStv Rewards,  Bw. Peter Amandus ambaye ni mfanyakazi wa TRA amepatikamna.

Mwaka huu DStv kwa kuridhishwa na ushirikiano mkubwa inaopata kutoka kwa wateja wake imeandaa kampeni mpya iitwayo DStv Rewards.

Kampeni hii itakuwa inawazawadia wateja wake Milioni 5,000,000/- kila wiki endapo mteja atalipia malipo ya mwezi kabla akaunti yake haijakatika.

Mpango huo umekuja Miezi michache tu, baada ya DStv kuzindua kampeni ya punguzo ya malipo ya Mwezi kwa asilimia kumi (10%) kwa vifurushi vyake vyote.

Hii ni kama moja ya zawadi zake kwa wateja endepo mteja atalipia  malipo ya mwezi kabla akaunti yake haijakatika.

No comments: