Wananchi wa kata ya Sasilo wilayani Manyoni Mkoa wa Singida wakifurahia baada ya kata hiyo Kukabidhiwa hundi ya Tsh 60 Mil iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania [TBL] kwa ajili ya uchimbaji wa visima 20 vya maji ambapo waliomba kupiga nayo picha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida, Fortunata Malya akitoa shukrani kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa kutoa msaada wa sh. mil 60 katika Kata ya Sasilo kwa ajili ya uchimbaji wa visima 20 vya maji. Hafla ya makabidhiano ilifanyika hivi karibuni katika kata hiyo.
Mkazi wa Kijiji Cha Sasilo Wilayani Manyoni Mkoa wa Singida Selebia Robert 51 mfugaji akiwa Nyumbani kwake pamoja na Familia yake kwenye pozi la picha huku wakiwa na vibuyu vya kuchotea maji na matumaini ya kupata maji Baada ya Kata yao kukabidhiwa Milion 60 na TBL kwa ajili ya Uchimbaji wa visima 20 vya maji vitakavyopunguza tatizo Hilo.
Meneja wa kampuni ya Bia Tanzania [TBL] Kanda ya Kusini, James Bokela akizungumza na wananchi wa Kata ya Sasilo, wilayani Manyoni, baada ya hivi karibuni kampuni hiyo kukabidhi msaada wa sh. mil 60 za kusaidia kuchimba visima vya maji.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania [TBL] Steve Kilindo akifafanua jambo mbele ya wananchi wa kata hiyo wakati alipoenda kukabidhi msaada wa 60 milion kwa ajili ya Uchimbaji wa Visima 20 vya maji.
Wananchi wa kata ya Sasilo wakifuatilia jambo wakati walipokuwa wakishuhudia upokeaji wa Msaada wa Tsh 60 mil zilizotolewa na TBL kwa ajili ya uchimbaji wa visima vya maji 20 makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Selakari ya mtaa na Mtendaji
No comments:
Post a Comment