Tangazo

May 31, 2013

African Barrick Gold (ABG) Tulawaka Gold Mine washerehekea Miaka Tisa ya Mafanikio 2004-2013

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Ziporrah Pangani (mbele), akiwa amesimama katika jukwaa dogo pamoja na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa African Barrick Gold (ABG), Greg Hawkins (kushoto) na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa ABG wa Tulawaka, Filbert Rweyemamu wakati wimbo wa taifa ukipigwa kabla ya kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na kikosi cha kampuni binafsi ya ulinzi ya KK Security wakati wa Sherehe za Miaka Tisa (2004-2013) ya Mafanikio ya mgodi huo, zilizofanyika mgodini hapo Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera hivi karibuni. Mheshimiwa Pangani alikuwa ni mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Ziporrah Pangani akikagua gwaride la kikosi cha KK Security.

Askari wa KK Security wakifanya maonyesho ya Field Craft.




Baada ya gwaride yalifuatia maonyesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tulawaka Gold Mine.

Meneja wa ABG Mahusiano ya Jamii, Stephen Kisakye (kushoto) na Ofisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Tulawa, Dorothy Dikurakule wakiwa timamu katika eneo lao la maonyesho.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Ziporrah Pangani (wa pili kulia), akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Dorothy Dikurakule Ofisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Dhahabu wa Tulawaka unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG), wakati wa maonyesho ya Sherehe za Miaka Tisa (2004-2013) ya Mafanikio ya mgodi huo, zilizofanyika mgodini hapo Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera hivi karibuni. Wanaoshuhudia (kulia) ni Rais wa ABG Mahusiano ya Umma, Deo Mwanyika na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Tulawaka, Filbert Rweyemamu. (wa tatu kulia).

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Tulawaka, Filbert Rweyemamu akisoma hotuba yake.

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa African Barrick Gold (ABG), Greg Hawkins akisoma hotuba yake.

Sehemu ya wafanyakazi wa Mgodi wa Tulawaka waliohudhuria sherehe hizo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Ziporrah Pangani akisoma hotuba yake.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Ziporrah Pangani (wa pili kulia), akikabidhi tuzo kwa mmoja kati ya wafanyakazi bora wa Mgodi wa Dhahabu wa Tulawaka unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG), wakati wa Sherehe za Miaka Tisa (2004-2013) ya Mafanikio ya mgodi huo, zilizofanyika mgodini hapo Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Filbert Rweyemamu (kulia) na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa African Barrick Gold (ABG), Greg Hawkins (wa tatu kulia).

Baada ya shamra shamra uliwadia wakati wa maakuli.

Professional MC. Mavunde  akiitambulisha kamati ya maandalizi ya sherehe hizo.

Usiku ulipowadia Skylight Band walishusha muziki wa nguvu na kukonga nyoyo za wana tulawaka.

Mzee Mfanyakazi wa mgodi huo alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta yupo jukwaani akiwasaidia kina Sony Masamba kusakata rhumba.

Kiongozi wa bendi ya Skylight, Aneth Kushaba 'AK47' (kulia), akiongoza safu yake kulishambulia jukwaa katika hafla hiyo ya jioni. Kushoto ni Mary Lucas na  Sony Masamba. Carolina mamaaaaaaa.........

Kwa kweli watu wote siku hiyo walikuwa na nyuso za furaha sana. Katikati ni Dk. Zumbi Musiba wa ABG Dar es Salaam.

Watu waliserebuka hadi majogooooo....

No comments: