Tangazo

June 11, 2013

BREAKING NEWS: MZEE TIMOTHY APIYO AFARIKI DUNIA

Mzee Apiyo (kulia) enzi za uhai wake akiwa na Mzee Sabodo
Taarifa zilizotufikai punde ni kuwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mzee Timoth Apiyo amefariki dunia usiku wa jana akiwa katika matibabu  katika Hospitali ya Mill Park nchini South Africa. Msiba upo nyumbani kwake Sitaki Shari - Ukonga jijini Dar es Salaam.

Tutazidi kuwajuza kadri tutakavyokuwa tukipata taarifa zaidi.

Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Mzee wetu Mzee Apiyo.
Amen

1 comment:

Anonymous said...

Kamwe mchango wake kwa Tanzania na kwa watu wake kwa ujumla usisahaulike. Watanzania tujifunze kuwaenzi wapendwa wetu hata wakiwa hai. R.I.P mzee Apiyo na pole kwa familia na marafiki zake