Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akipokea Salamu za heshima kutoka kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya.
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akikagua wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika
chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya.
**************************
JUMLA ya Askari 984 wa Jeshi la
Magereza, wanaume 845 na wanawake 139
wametunukiwa Vyeo vya Ukoplo
baada ya kuhitimu mafunzo ya Uongozi daraja la Kwanza kozi namba 20 katika Chuo
cha Magereza Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Vyeo hivyo vilitolewa na
Kamishina wa Fedha na Utawala Gaston Sanga kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa
Magereza katika Sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zilizofanyika katika
Viwanja vya Chuo hicho leo Juni 7, Mwaka huu.
Akizungumza katika mahafali
hayo, Kamishina wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga amesema Askari wa
Jeshi la Magereza Nchini wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili,
taratibu na kanuni za kazi kwa kufuata uwajibikaji, unyenyekevu, ukakamavu,
ujasili, upendo, ushirikiano, uvumilivu, uaminifu na nidhamu.
Kamishina Sanga amesema
Maaskari wanapaswa kuzingatia elimu waliyopewa wakati wa mafunzo ili wakawe
mfano kipindi cha utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na
kuwaongoza wenzao ambao hawakupatiwa elimu kama yao.
Aidha amewaasa kutowatesa
Wafungwa walioko magerezani bali kuwahudumia kwa kuzingatia kuwa wanamhudumia
binadamu kama walivyo wao na siyo
kuchukua nafasi ya kuwanyanyasa bila kuogopa haki na Stahili za binadamu
japokuwa ni wafungwa.
No comments:
Post a Comment