Mwana dada nguli katika Sanaa ya Muziki nchini Tanzania na Mshindi wa Tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike mara kadhaa na mwaka huu, Judith Wambura a.k.a Lady JayDee a.k.a Jide a.k.a Mama somefood a.k.a Komando hatimaye usiku wa kumakia jana alifanya show yake kali ya kutimiza miaka 13 katika sanaa ya Muziki nchini.
Show hiyo kali na ya aina yake ambayo awali ilikuwa ifanyike Mei 31, mwaka huu katika ukumbi wa Nyumbani Lounge Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Msanii mwenzake Albert Mangwea ilifanyika jana licha ya kuwa palitokea msiba wa msanii mwingine Langa.
Jide ambaye alisindikizwa na wasanii kibao akiwepo Mkongwe Hamza Kalala, Prof. J, Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye ni Mkongwe katika mziki wa Kizazi kipya Joseph Mbilinyi 'Sugu', Juma Nature na wengine wengi.
Watu wakiwa wamefurika kiasi cha kukosa kupenyeza mguu Lady JayDee alitumbuiza jukwaani kwa nyimbo zake kadhaa za zamani ambazo zilionesha kukonga vilivyo nyoyo za mashabiki na wapenzi wake ambao sasa anawapeleka kwa staili ya Nyoka Mkali ANACONDA.
Sugu akiwa jukwaani. |
Wanaume Halisi Jukwaani. |
Mambo ya Anaconda jukwaani. |
Furaha kwa kwenda mbeleeeeeeeeeeee. |
Jay Dee akikusanya fedha alizotunzwa na mashabiki wake na kumkabidhi mama yake. |
Lady Jay Dee akiwa katika pozi na mama yake mzazi. |
Lady JayDee akiimba na Prof. J kibao chake cha Joto Hasira. |
Judith Wambura akiimba na Mkongwe Hamza Kalala. |
Prof J akikamua jukwaani sambamba na DJ Choka. |
No comments:
Post a Comment