Tangazo

June 3, 2013

SALSHIA ISDORE NDIYE REDD'S MISS GEITA 2013


Mshindi wa taji la Redd’s Miss Geita 2013, Salshia Isidore (katikati) akiwa mwenye furaha wakati wa kupiga picha ya pamoja na warembo wqenzake Stella Magerezi (kulia) aliyeshika nafasi ya pili na Mshindi wa tatu wa shindano hilo, Nurieth Rashid. Salshia aliwashinda warembo wenzake 12 waliokuwa wakiwania taji hilo pamoja nae.
******      *******
Na Father Kidevu Blog, Geita
MREMBO Salshia Isidore amechaguliwa kuwa Redd’s Miss Geita 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 12 katika shindano lililifanyika Jumamosi  Juni 1,  kwenye ukumbi wa Desire uliopo mjini Geita.

Wengine walioingia nafasi ya tatu bora ni pamoja na Nurieth Rashid aliyeshika nafasi ya tatu na Stella Magerezi alishika nafasi ya pili.

Katika shindano hilo lililosindikizwa na burudani safi kutoka kwa msanii Baby Madaha na Bob Haisa huku mgeni rasmi akiwa ni Mbunge wa Viti Maalum wa Geita Vicky Kamata.

Washindi hao watatu watawakilisha mkoa wa Geita kwenye shindano la Kanda ya Ziwa ili kuwapata washiriki watakaoenda ngazi ya taifa.

Akizungumza na washindi pamoja na warembo wengine kwa ujumla Vicky aliitaka jamii ya watu wa Geita kuyatambua mashindano hayo kuwa ni muhimu na yanasaidia suala la ajira.

Alisema kuwa kupitia mashindano hayo kuna mengi ambayo yanaweza kufanyika kwa kuwa mashindano hayo ni fursa ya kuzungumza na wananchi kuielezea masuala mbalimbali ya kimaisha.

“ Najua kwa sasa hata katika Bunge hili la bajeti kuna mengi ambayo tumeyajadili na kuyapitisha kwa ajili ya vijana na hasa pia kupitia sanaa na hivyo mashindano kama haya yanahusika kabisa” alisema Vicky.

Naye mwandaji wa shindano hilo alisema kuwa washindi hao mshindi wa kwanza amepewa laki tatu, huku wa pili amepewa laki mbili na wa tatu laki tatu.

 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja.
 Wanyange walioshiriki shindano la Redd's Miss Geita 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jukwaani.
Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoani Geita, Vicky Kamata (kulia) akitoa nasaha zake kwa washindi na warembo wote walioshiriki shindano hilo.

No comments: