Tangazo

July 9, 2013

WASHINDI TABORA MARATHON WAULA

Na Mwandishi Wetu, Tabora.

WASHINDI wa mbio za Tabora Marathon 2013 wa mbio za kilomita 15,wanawake na wanaume 21,wamepata ofa ya kwenda kituo cha Holili Youth Athletics Clubs (HYAC), kwa mafunzo ya miezi sita.

Mkurugenzi wa kituo hicho, Domisian Genandi, aliyasema hayo kupitia kwa Mshauri wa Ufundi wa Tabora Marathon, Tullo Chambo, akieleze kufurahishwa na mbio hizo.

Genandi alisema kuwa, kituo chake ambacho mlengo wake ni kuinua vipaji vya vijana, kimeamua kuchukua vijana hao ili kwenda kwenye mafunzo ya miezi sita ili kuweza kutoa fursa ya kupata mazoezi ya kutosha kuliko kusubiri kipindi cha mashndano ya mbio hizo tu.

Vijana hao ambao wanatarajia kunufaika na ofa hiyo ni washindi wawili katika mbio za Nusu Marathon kwa wanaume na Kilomita 15 kwa wasihana.

Washindi hao ni Grace Jackson ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Mwinyi na Maombi Elisha mkazi wa Ng`ambo mjini hapa.

Kwa upande wa wanaume waliopata fursa hiyo ni Jabu Mwandu mkazi wa Igunga na Dickson Mkami mkazi wa Uyui.

Genandi aliongeza kuwa, kituo chake alikianzisha mwaka 2010 kikiwa na watoto sita na kwa sasa kina watoto 15.

 Alisema ameanzisha mbio zitakazohusisha mita 200, 400, 1,500, 5,000, 8,000 na 10,000 kila wilaya mkoani Kagera, ambako washindi watatu kila mbio hizo wataungana kwenye kituo chake na maandalizi yote yameshafanyika kwenye klabu yake kuwapokea.

Alisema, mashindano hayo mkoani Kagera aliwasiliana na uongozi wa mkoa idara ya michezo na kwamba klabu yake imekuwa ikipata vijana kupitia vyama vya riadha mkoa hadi taifa.

Alisema klabu yake imekuwa ikipata mafanikio hasa kutokana na mipango aliyonayo na mara kadhaa anapowaingiza kwenye mbio za kimataifa wamekuwa wakifanya vyema.

Hata hivyo, Genandi alisema kuwa, amekuwa akipata changamoto kadhaa ikiwemo kukosekana kwa wafadhili, lakini amekuwa akiendesha kituo chake kwa kujitolea na ametoa wito kwa wadau kumuunga mkono.

No comments: