Tangazo

July 9, 2013

Ziara ya Waziri Mkuu Pinda katika Mikoa ya Iringa na Njombe

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsaidia kutembea mtoto, Asante Mtega wa kituo cha kulea na kuwasaidia watoto wenye ulemavu cha Inuka kilichopo  Mayale Iringa wakati alipokitembelea  Julai 8,2013. Katikati ni Mkewe Tunu na (kushoto) ni Askofu wa Kanisa Katoliki Njombe, Alfred Maluma. (picha na Ofisiya Waziri mkuu)

Waziri mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa  Kijiji cha Igwachanya  wilayani Wanging'ombe  wakati alipoingia kijijini  hapo akiwa  katika ziara ya mkoa wa Njombe Julai 8, 2013. Kushoto ni Mkewe Tunu na Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Estelina Kilasi  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe, Alfred Maluma wakiweka jiwe la msingi la Chuuo cha Kilimo na Mifugo cha Mare - Mayale katika wilaya ya Wanging'ombe, Julai 8,2013. Kulia ni mkewe, Tunu.  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe,Alfred Maluma  kabla ya kuwaslimia wananchi  katika misheni ya Ilembula wilayani Wanging'ombe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Julai 9,2013. (Picha na Ofisi ya WaziriMkuu
 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Igwachanya Makao makuu ya wilaya ya Wanging'ombe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Julai 8, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda akipokea maua kutoka kwa Skauti wakati alipoingia kwenye  Wilaya  ya Njombe akiongozana na Waziri Mkuu  katika ziara ya mkoa wa Nombe Julai 8, 2013.  Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wasanii wa Njombe wakitumbuizaa wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipoingia wilayani Njombe kwa ziara ya Mkoa wa Njombe Julai 8,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


No comments: