Tangazo

August 19, 2013

NBC yazindua Huduma ya Mawasiliano ya papo kwa papo ya wateja (Hotline Service)

Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Maharage Chande akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya mawasiliano ya papo kwa papo (Hotline Service) kati ya mteja wa benki hiyo na maofisa wa benki nhuduma itakayopatikana ndani ya matawi ya NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Maharage Chande (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha benki hiyo, Jane Dogani (kushoto), wakifurahia wakati mmoja wa wateja wao, Amin Juma (katikati) akijibiwa swali alilouliza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.

Kwa kupitia Holine Service ya NBC mteja kama huyu Bwana Amin Juma sasa anaweza kujibiwa maswali yake akiwa ndani ya tawi la benki hiyo. Anaweza kuuliza, kutoa malalamiko ama pongezi au dukuduku lolote naye atapata majibu yake hapo hapo kutoka kwa maofisa wa benki hiyo wanaofanya kazi masaa 24 katika kituo cha mawasiliano (Contact Centre) cha NBC. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa NBC, Maharage Chande.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Benki ya NBC, Jane Dogani akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Hotline Service inayomwezesha mteja wa NBC kuuliza maswali yake moja kwa moja kwa ofisa wa benki hiyo awapo ndani ya tawi la benki.

Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, Eddie Mhina akiongoza shughuli za uzinduzi wa huduma ya Hotline Service ya Benki ya NBC katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam.

No comments: