NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (pichani), amewataka waganga wa tiba asili washirikiane na wataalamu wa utafiti ili kuwezesha upatikanaji wa dawa bora na salama.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri huyo wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya siku ya tiba ya asili ya mwafrika ambayo huadhimishwa kila mwaka Agosti 31, lakini mwaka huu hayakufanyika kutokana na uhaba wa fedha. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika mwakani kipindi katika hicho.
“ Tanzania tunayo mitidawa mingi na mingi haijafanyiwa kazi katika utafit na kuweza kubaini uwezo wa kutibu magonjwa mbailmbali tatizo lililopo ni jinsi gani mitidawa hiyo inweza kufanyiwa utafiti na kuwa dawa bora na salama kwa watumiaji kwa kuziwekea mifumo ya huduma za afya ili kila mwenye kuhitaji aweze kuzipata,” alisema Dk. Mwinyi .
Dk. Mwinyi aliwataka waganga hao kushirikiana na watafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Taasisi ya Utafiti wa Dawa za Asili iliyokpo katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shiriki- (MUHAS).
Aliongeza kuwa waganga wote wa tiba asili na tiba ya kisasa wanatakiwa kufanya kazi kwa kuelewana ili kuwezesha kupata taarifa za awali kabla ya utafiti kamili kufanyika.
Aliitaja kauli mbiu ya maadhimisho hayo kuwa ni ‘ Tiba Asili : Utafiti na Maendeleo’ kuwa inalenga kutoa majukumu kwa waganaga wa tiba asili na tiba mbadala katika sula zima la utafiti. Pili inatoa changamoto juu ya uendelezaji wa taarifa za utafiti wa mitidawa katika kutafuta dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali.
Aidha aliwahimiza waganga wa tiba asili kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na huduma za afya.

No comments:
Post a Comment