Tangazo

January 21, 2014

CCM na CHADEMA wazindua kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kiboriloni

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanajro, Iddi Juma, (aliyeshika kipaza sauti), akimnadi mgombea wa CCm katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani, Wlly Adriano katika uchaguzi uzinduzi wa kampeni za uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo lililoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwanbi wa Kata ya Kiborloni, Vincent Rimoy, aliyefariki dunia ghafla Novemba 6 mwaka
jana.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na Mwandishi Wetu, Moshi

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mwishoni mwa wiki walifanya uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi  mdogo wa udiwani katika kata ya Kiboriloni liliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Vincent Rimoy (CHADEMA), aliyefariki ghafla Novemba 6 mwaka jana.

Wa kwanza kufanya uzinduzi ni Chadema, waliozindua kampeni yao kwa mbwembwe wakimtambulisha mgombea wao, Frank Kagoma ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi, uzinduzi ulioongozwa na viongozi
mbalimbali wa ngazi za juu wa chama hicho mkoani hapa akiwemo mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Filemon Ndesamburo.

Wakizungumza katika Nyakati tofauti katika uzinduzi huo uliofanyika, Jumamosi ya Januari 18, mwaka huu, katika stendi ya kidia, viongozi wa Chadema walianza kumnadi mgombea wao ambap[o walimtaja kama mtu sahihi ambaye anaweza kuendeleza mapambano ya chama hicho ndani ya baraza la madiwani kupinga ufisadi na uonevu katika manispaa ya Moshi.

Meya wa Manispaa ya Moshi, Jafari Michael, aliwataka wananchi wa kata hiyo kumchagua mgombea wa Chadema kwani ndiye mwenye uwezo wa kutekeleza yale yote aliyoyaanzisha Marehemu Rimoy ndani ya kata hiyo na baraza la madiwani.

“Wananchi wa kiboriloni msidanganyike, chaguo la kweli katika maendeleo ya kata hii ni Kagoma, katika kipindi chake kama mwenyekiti Kagoma alifanikiwa kuvunja magenge yote ya ujambazi na sasa mnatembea

vifua mbele bia wasiwasi, tupeni kagoma tuendeleze moto wa Chadema ndani ya Baraza la Madiwani, tupeni kagoma tukamalizie kazi aliyoianzisha Rimoy,” alisema Rimoy.

Naye Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Filemona Ndesamburo alisema kazi  ya kuleta maendeleo katika kata hiyo na mkoa kwa ujumla  unaweza kufanywa na watu makini wenye uthubutu kama alivyo na uthubutu Mgombe wa kiti hicho, Frank Kagoma.

Kwa upande wao, Chama cha Mapinduzi CCM, waliofanya uzinduzi wao juzi, kwa kumtambulisha mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya CCM, Willy Adriano walisema Maendeleo ya kata ya Kiborloni ni zaidi ya itikadi za siasa na kuwataka wananchi wa kata hiyo kufanya uamuzi sahihi.

Akizungumza na maelefu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya stendi ya Kidia, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi alisema wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitafuta madaraka kwa njia mbalimbali, ikiwemo  kufanya vurugu na maandamano.

 “Unajua ukisikia nchi fulani ina maendeleo kiuchumi, kisiasa na mambo mengine ni kwa sababu kuna amani, kwa hiyo hili jambo ndugu zangu ni muhimu sana kulizingatia ili kutuwezesha kuendelea na kazi zetu za
kijamii vizuri” alisema Kazidi.

Kwa upande wake Mchumi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu, aliwataka  vijana kutokuuza shada zao za kupigia kura kwani kufanya hivyo ni kuuuza maendeleo yake.

Aidha Matemu aliongeza kwa kusema  kuwa siasa bila maendeleo hakuna kujenga msingi wa kuleta maendeleo, na kuwataka wananchi wa kata ya kiboriloni kuchagua Willy Adriano ili aweze kuwawakilisha katika baraza la madiwa la Manispaa ya Moshi.

Naye Mgombea udiwani kwa tiketi ya chama hicho, Willy Adriano, alisema Siasa za Tanzania haziwezi kupiga hatua endapo wananchi hawatabadilika na kuacha tabia ya kuchaguana kwa kuangalia kigezo cha itikadi za kisiasa.

Uchaguzi mdogo wa udiiwani  katika kata ya Kiboriloni uunarajiwa kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo lililoachwa wazi kufuatia kifocha aliyekuwa diwani wa kata hiyo kwa tikiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Vincent Rimoy.

Rimoy ambaye alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi, alifariki dunia ghafla, Novemba 6 mwaka jana, baada ya kudondoka akiwa shambani kwake eneo la mandaka wilaya ya Moshi.

No comments: