Tangazo

March 5, 2014

Tanga Cement yaahidi kuendelea kudhamini Kili Marathon

 Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Saruji Tanga (TCCL) wakishiriki mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro jana. Tanga Cement ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mbio hizo ikitoa maji ya kunywa na kupoozea mwili kwa wakimbiaji.
Mmoja wa wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za Kilomita tano za Vodacom Fun Run, Tsadia Jessie Bercuvitz (5) raia wa Uingereza akipewa sponji lenye maji kwa ajili ya kupunguza joto na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Saruji Tanga, Mtanga Noor wakati wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon mjini Moshi, Kilimanjaro juzi.
Waziri wa Habari  Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo ,Dkt Fenella Mukangara akimpa cheti Meneja Mauzo wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Leslie Massawe (wa pili kulia)  kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon yaliyomalizika juzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Kushoto kwa Waziri Mukangara ni Waziri wa Mifugo, Dk Titus Kamani.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga, Changwa Mjella (kulia) na Mtanga Noor (katikati) wakimpa maji mmoja wa wakimbiaji wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro juzi.

No comments: