Tangazo

April 23, 2014

KATAA UNENE FAMILY (KUF) YAWAKEMEA WATU WANAOTUMIA PICHA ZAO KWENYE BIASHARA ZAO ZA MADAWA YA KUPUNGUZA UZITO

Kiongozi wa Kikundi cha Kataa Unene Family (KUF) ambaye pia ni mwandishi na mtangazaji wa Televison ya Taifa (TBC1), Angella Msangi amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia picha zao ili waweze kuuza biashara zao za madawa ya kupunguza uzito.
Akizungumza na Kajunason Blog kwa masikitiko makubwa, Kiongozi huyo alisema kuwa kuna wafanyabiasha ambao si waaminifu wamekuwa wakichukua picha zao katika mitandao ya jamii na sehemu nyingine na kutangazia biashara zao kuwa hao wametumia dawa zao na wamepungua.
Pichani ni Kiongozi wa Kikundi cha Kataa Unene Family (KUF) ambaye pia ni mwandishi na mtangazaj wa Televison ya Taifa (TBC1), Angella Msangi akiwatambulisha wanakikundi wenzake mbele ya Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda. Hii ilifanyika mwishoni mwa mwaka jana mara baada ya kushiriki Mbio za Uhuru. (Picha na Maktaba.)

“Kiukweli nimechukizwa na tabia hii ambayo kwa sasa imesambaa kwa wafanyabiashara wengi wa madawa ya kupunguza uzito, wanachukua picha zetu na kusema wametuuzia dawa zao na tumepunguza uzito… Naomba watambue kuwa sisi tunafanya mazoezi na ulaji bora (diet) ndiyo maana tunapungua uzito", alisema Angella.

Aliongeza kuwa kwa sasa wameshawasiliana na mwanasheria wao na watawafikisha mbele ya sheria watu wote ambao si waaminifu wanataka kujipatia kipato kwa njia ya udanganyifu wa picha za watu.
Wanakikundi wa KUF wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Fenella Mkangala. Hii ilifanyika mwishoni mwa mwaka jana mara baada ya kushiriki Mbio za Uhuru. (Picha na Maktaba.)
Hili ni moja ya tangazo lililotumiwa na wafanyabiashara hao kuonyesha jinsi bidhaa zao zinavyopunguza unene wakati si kweli, huyu ni mmoja ya wanachama wa KUF.
 
Kundi la KUF linawanachama wapatao 50 ambao hukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja huku wakihamasishana kila muda kufanya mazoezi na kujitahidi kula vyakula vitakavyojenga mwili.

No comments: