Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa
nyumba 60 za makazi ya watu zinazojengwa na Shirika la Nyumba ya Taifa katika
Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Katavi Ndugu Nehemia Msigwa juu ya miradi ya ujenzi
wa nyumba itakayofanyika ndani ya mkoa wa Katavi.
Pichani ni Michoro ya Nyumba zitakazojengwa mkoani Katavi na Shirika la Nyumba ya Taifa,ambapo wilaya ya Mlele ,Shirika la Nyumba linajenga nyumba 60 na zitachukua miezi nane kukamilika.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Rutengwe akizungumza mbele ya
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi
la uzinduzi wa nyumba 60 zitakazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
katika wilaya ya Mlele.
Meneja
wa Huduma za Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa Ndugu Muungano Saguya
akizungumzia namna Shirika la Nyumba lilivyojipanga katika kuboresha makazi ya
watu katika mkoa wa Katavi.
Picha na Adam Mzee
No comments:
Post a Comment