Wajumbe wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) wakiendelea na Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Mkutnao huo umefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Peter Ilomo (katikati mwenye tai nyekundu).
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Peter Ilomo akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Irene Isaka (kushoto) akizungumza kwenye Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko,Mitaji na Dhamana (CMSA),Nasama Masinda akieleza jambo wakati Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA),Oaitse Ramasedi (wa tatu kushoto) akiongoma Mkutano huo unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI wa Mfuko
unaosimamia mifuko ya hifadhi za Jamii nchini (SSRA) , Irene Isaka ametoa
wito kwa wanachama wapya kujiunga kwa wingi kwenye mifuko hiyo kwa
sababu muda si mrefu serikali itaweka uwiano wa mafao sawa kwa mifuko
yote.
Isaka alisema hayo
jana katika mkutano wa 32 ambao unazikutanisha nchi wanachama wa
SADC unaendelea jijini Dar es Salam.
“ Tukiwa katika
mkutano huu tunaweza kujifunza mambo mengi kutoka kwa wenzetu wa SADC
huku na wao wakijifunza mambo kadhaa kutoka kwetu kwani zipo baadhi ya
nchi ambazo hazina mfuko mkuu kama SSRA ambao ndio mfuko mama unaosimamkia kazi
na utendaji wa mifuko mingine ya kijamii” alisema Isaka.
Aliongeza kwa
kusema kuwa hivi sasa kumezuka mtindo kwa badhi ya mifuko ya jamii kujipigia
debe,hilo suala ni zuri ila jambo ambalo SSRA tunapingana nalo ni la
kunyang’anyana wanachama,hilo siyo jambo zuri hata kama wako kibiashara”alisema.
Aliongeza kwa
kusema kuwa natoa wito kwa mifuko mbalimbali ya kijami kuwa na ushindani
endelevu wa kusaidia wanajamii ambao ndiyo wanachama wao.
Aliongeza kwa
kusema kwamba SSRA wakiwa wasimamizi wakuu wa mifuko ya hifadhi za jamii wako
katika mazungumzo na serikali kuhusu mifuko yote iwe na kikokotoo kimoja
kitakachoweka uwiano sawa.
Akizungumzia kuhusu
mifuko ya jamii kuwa na kikokotoo kimoja amesema hatua za awali tayari
zimekamilika na wameshakusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali huku wakiwa
wameshapata Baraka za serikali.
Naye Kamishna
wa Bima nchini, Israel Kamuzora alisema mwaka 2009
kulikua na watanzania idadi ya asilimia 6.3 tu ambao walikua wakitumia
huduma ya Bima tofauti na hivi sasa ambapo mwamko umekuwa mkubwa miongoni mwa
watanzania kwa kuona umuhimu wa kukata bima ambazo ni za afya, biashara,
magari na nyinginezo.
Akizungumzia
watanzania walichojifunza katika mkutano huu kwa nchi zingine,Kamuzora alisema
kwamba ni kweli Tanzana iko nyuma kwa pande wa matumizi ya Bima lakini
pia tuko mbele kwa nchi kama Msumbiji, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC),Lesotho na nyinginezo.
Amesema hivi sasa
Bima hawacheleweshi malipo kwa watu wanaodai huku akitoa wito kwa
wananchi kupeleka madai huku wakiwa na vielelezo vya kutosha.
Alivija
vithibitisho hivyo kuwa ni kutoa tarifa haraka zilizokamilika baada ya kupata
ajali ikiwa ni ripoti ya polisi,ushahidi wa kipato cha muhusika anachokipata
kwa siku ili wao waweze kukokotoa hesabu na muhusika aweze kulipwa.
Aidha alisema
kwamba watanzania wengi hawana ajira za kudumu jambo ambalo hukwamisha hesabu
za kuharakisha malipo kwa wale ambao hupatwa na ajali na kushindwa kuendelea na
kazi zao kama ilivyokua awali.
Wakati huohuo
Mkurugenzi wa Masoko ya Mamlaka ya Masoko,Mitaji na Dhamana (CMSA),Nasama
Masinda alisema kwamba Tanzania hatuko katika hatua mbaya huku akizitaja
nchi kama Afrika Kusini na Kenya zikiwa zImepiga hatua kubwa
“Watanzania
wamekuwa nyuma huku wakikosa mwamko wa kuchangia katika masoko ya mitaji,
hivyo basi tumeweka mikakati ya kutoa elimu kwa umma katika miaka
mitano ijayo ili waweze kunufaika na soko la mijati ili nchi iweze kupiga hatua
kama jinsi walivyo wenzetu.
Alitolea mfano nchi
jiani ya Kenya ambayo ilianza kuwa a soko la mitaji mwaka 1950 huku Tanzania
ikianzisha soko hilo 1998.
Mgeni rasmi katika
mkutano huo wa sekta ya fedha, soko la mitaji na mifuko ya jamii (CISNA)
alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Peter Ilomo.
Ilomo amewataka
wajumbe wa mkutano huo wa CISNA watoke na lengo moja la kukuza uhusiano na kuwa
na maazimio ya kukuza masoko yao ya mitaji ikiwa ni katika kuvutia wawekezaji
waje kununua masoko katika nchi za SADC kwani hiyo ni njia moja wapo ya kukuza
uchumi wa Afrika na mwekezaji yeyote hufuata nchi ama umoja wenye nguvu.
“Nchi za SADC
zijipange kuwa na ushindani katika nyanja zote za mifuko ya jamii, soko la
mitaji na bima ili kuleta maendeleo” alisema Ilomo.
Nchini
zilizoshiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na Zimbabwe,Botswana,Tanzania,Angola,Lesotho,Zambia,Malawi,Afrika
Kusini,Namibia,Msumbiji,Mautitius na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment